Rais Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinto ambaye yuko nchini kwa ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na taasisi yake ya Clinton Foundation katika nchi kadhaa za Afrika |
Katika msafara wa Mhe Bill Clinton kuna mastaa kadhaa wa sinema basketball ambao wameongozana na Rais huyo mstaafu wa Marekani aliye katika ziara ya kikazi kukagua na kuendeleza kazi za maendeleo zinazofanywa barani Afrika na taaisis yake ya Clinton Foundation. Pichani juu kulia ni mcheza sinema nyota Dakota Fanning akiongea na mcheza sinema mwingine nyota Jesse Eisenberg na nyuma yao aliyekwenda juu ni mcheza basketball katika NBA Brook Lopez
Jesse Eisenberg na Dakota Fanning wakishuhudia utiwaji saini wa mkataba wa maelewano kati ya Serikali ya Tanzania na tasisi ya Clinton Foundation Ikulu jijini Dar es salaam
Ankal akiwa na Jesse Eisenberg
Ankal akila pozi na Brook Lopez ambaye kenda hewani
kama Hasheem Thabeet
Hawa wamarekani wanazidi kumuongezea hasiri mheshimiwa sana rais Kagame.
ReplyDeleteYano bado Jimmy carter na Bush baba ili kukamilisha idadi ya marais wote wa USA wanoishi.
ReplyDeleteWhat has this to do with Kagame? These are just planned visit and Clinton will visit Rwanda as well.
ReplyDeleteNadhani mdau hapo juu Jimmy carter ameshafika Tanzania miaka ya sabini. Naomba wadau mnirekebishe katika hili kama nimekosea. Bado Bush baba tu.
ReplyDeleteSasa Tanzania imejulikana Duniani, hata watalii watazidi sana mwaka huu, kwasababu Rais Kikweti ameitangaza nchi kwa ujio wa Rais Obama.
ReplyDeleteHuyo Jesse ndiye yule star wa movie ya Facebook aliyeigiza kama Zuckberg eenh??
ReplyDeletekuingia ni rahisi kutoka sasa ngoja tutaona mwisho wake hatimaye litakuwa shamba la wamarekani nyanya ,kabeji mchicha utatoka hapa kwenda marekani kama ilivyokuwa zimbabwe shamba la uingereza.cha msingi watu wamilikishwe ardhi ili mwekezaji aungane na wazawa sio mwekezaji amilikishwe rasilimali
ReplyDeleteBush tayari au unamsema Bush baba'ke? Duu yaani Mungu kaumba binadamu kutofautiana! Ankal huyo jamaa unamfikia tumboni !! Kweli si mchezo!! Teh teh teh!!
ReplyDeleteHii si bure lazima tujipange kwa kichwa. Unajua tuwe smart ktk kushirikiana na Marekani wao wameshaamua hapo wanatoa msisitizo tu. Tukijinga vizuri kuhakikisha kuna win-win tutafika nao mbali,wenzetu S.Korea, Japan Na China wamefanikiwa kihivyo. Elimu ipewe kipao mbele ili kuandaa skilled labour, viongozi tuachana na bogus agreements ya akina Chenge, tuachane Na mentality ya misaada ambayo inakufanya uwe weak partner Bali tuangalie kwa makini kwa kila hatua nchi inafaikaje. Tuhusishe wazalendo ktk majadiliano ya mikataba, kunahaja ya kuunda timu maalumu ya kitaifa kupitia rasimu za mikataba ya kiuwekezaji kabla ya kusainiwa. Timu hiyo ijumuishe na wakereketwa kutoka hata kwenye vyama vya upinzani ili tusikosei mahali, jamani tunatakiwa kujenga nchi yetu kwa umakini ukubwa na tuwe na mtazamo wa miaka 500 ijayo. Hizo rasilimali zilizopo zitakapoisha na hatujafanya maendeleo yakueleweka basi taifa litadharauliwa mno duniani. Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteAnkal chini ya mti wa mbuyu..
ReplyDeleteMdau wa No.1 na No.3 Raisi Kagame ametopoza umaarufu ktk Jumuiya ya Kimataifa kwa Kitendo chek cha siri cha kushiriki ule Ujambazi Mahsariki ya Kongo kwa kuwasaidia M-23.
ReplyDeleteLicha ya Maendeleo anayosifiwa kuleta nchini kwake na mafanaikio lakini nyuma yake pana Kivuli kichafu.
Hapo ndio pale unakuta Kiongozi Mkuu wa Dini anashiriki Ujambazi!
Ikiwa unachakuuza na Mmarekani basi atashirikiana na wewe. Ukiwa huna kitu atakwambia bye!!
ReplyDeleteNilifikiri Ankal ame-shrink kwa ajili ya swaumu.
ReplyDelete